Fatma Karume Afunguka Sakata la Pierre wa Liquid na Makonda

Rais wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS), Fatma Karume amesema kuwa Watanzania wamemtetea Piere kwakuwa ni haki ya binadamu kuishi maisha anayoyataka yeye, na wanaombeza wanakosea.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Karume amesema kuwa, anachokifanya mchekeshaji huyo ni sahihi na havunji sheria za nchi.

"Piere mimi nimechelewa kumjua kwani sijamjua mapema hadi pale alipoitwa wa hovyo", amesema Karume.

Akizungumzia namna Piere alivyoambiwa kuwa ni moja kati ya watu wa hovyo, amesema kuwa anatakiwa kumshukuru Makonda kwakuwa amefanikiwa kumpiga teke lililomuongezea hatua.

Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kutoa kauli ya kukosoa tabia ya watu kuvipa muitikio mkubwa vitu visivyo na msingi, akitolea mfano mchekeshaji huyo aliyejizolea umaarufu kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii.

Katika hafla iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambayo ilikuwa na malengo ya kutokomeza ziro katika wilaya hiyo, Makonda alisema kwamba watu wa 'hovyo' kama Pierre hawapaswi kupewa nafasi kwenye vyombo vya habari, hali iliyozua gumzo kubwa.

Miongoni mwa kauli hizo, Makonda alisema,"Wakina mama kama hawa wanaojituma na kuhangaika kwa ajili ya watoto, wao ndio tuwape kipaumbele, sio hawa walevi walevi, yaani unakuwa na taifa ambalo watu wa hovyo ndio wanakuwa maarufu”.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad