Godbless Lema Anena Kuhusu Adhabu Yake, 'Sitanyamaza Hata Mauti'

Godbless Lema Anena Kuhusu Adhabu Yake, 'Sitanyamaza Hata Mauti'
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema adhabu aliyopewa na Bunge ya kutohudhuria mikutano mitatu ni kitu kinachompa nguvu kwenye mapambano dhidi ya kudai haki.

Mapema leo Kamati ya Bunge ya Kinga, Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Mbunge huyo  kwa kudharau Bunge kwa kuita Bunge ni dhaifu na hivyo kamati imeazimia Lema kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia leo.

"Nimesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge mpaka  January 2020.Moyo wangu una amani sana,kwani mahusiano yangu na HAKI yanaendelea kuimarika zaidi. Nawatakia Wabunge wenzangu kazi njema katika wajibu huu,sitanyamaza hata kama adhabu itakuwa ni mauti," ameandika Lema kwenye mtandao wa Twitter.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku moja kupita tangu Bunge kuazimia kumsimamisha mikutano Miwili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kutokana na kukiri kuunga mkono kauli ya CAG ya kusema mbunge ni dhaifu ikiwa ni mara yake ya nne kutenda makosa hayo ya kulidharau Bunge na kupewa adhabu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad