SiaaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa kuna mama alijitokeza jana na kusema kuwa mtoto wake amelawitiwa, hivyo aliwaagiza watu wakafuatilie wakamkuta Gereza la Ruanda anatumikia kifungo cha maisha.
Kufuatia sakata hilo, Rais Magufuli ameagiza Hakimu Mteite aliyekuwa anaendesha kesi hiyo jina lake lipendekezwe kwa Jaji Mkuu ili ateuliwe kuwa Jaji.
"Kuna Mama alijitokeza jana kuwa Mtoto wake amelawitiwa, watu wangu wakafuatilia wakamkuta aliyelawiti yuko Gereza la Ruanda anatumikia kifungo cha maisha, nampongeza Hakimu Mteite naagiza jina lake lipendekezwe kwa Jaji Mkuu ili ateuliwe kuwa Jaji," amesema Rais Magufuli.
"Naagiza jina la Hakimu Mkazi Mteite lipelekwe kwenye mapendekezo kwa Jaji Mkuu kwa majina yatakayokuja kwa watu wa kuteuliwa Ujaji nae awepo jina jina lake."
Ameyasema hayo leo Aprili 27 katika mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Sabasaba wilaya ya Chunya mkoani Mbeya ikiwa ni muendelezo wa ziara yake mkoani humo.