Hazina yadaiwa kupora fedha

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Zuberi Kabwe, ameitaka serikali kuzingatia Sheria na Katiba kuhusu Fedha za Taasisi ambazo zimetengwa kisheria lakini hazina imekuwa ikizitumia bila kufuata taratibu.

Zitto ameyasema hayo wakati akifanya uchambuzi wa ripoti iliyotolewa na Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, CAG, Prof Mussa Assad.

Zitto ameeleza kwamba kwa mwaka wa fedha  2017/18, CAG amebaini jumla ya shilingi 678 bilioni zilizokusanywa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kwa niaba ya taasisi nyingine hazikuhamishwa kwenda kwenye taasisi husika, na badala yake zilihamishiwa kwa Katibu Mkuu wa Hazina.

Zitto ameongeza kwamba Licha ya fedha hizo kuchukuliwa na hazina, bado huko hazikuonekana kwenye ukaguzi kama sheria inavyotaka.

"Fedha zilizoporwa na hazina ni pamoja na shilingi 169 bilioni za Shirika la Reli, shilingi 168 bilioni za Wadau wa Korosho nchini na shilingi bilioni 16 za Wakala wa Umeme Vijijini (REA). CAG kwa mara nyingine tena amependekeza sheria iheshimiwa kuhusu matumizi ya fedha hizi za Taasisi mbalimbali".

Ameongeza, "kwenye ripoti ya CAG ya mwaka 2016/17 kiasi cha shilingi 2.2 trilioni za mamlaka mbalimbali nchini hazikurejeshwa kwenye mamlaka husika mara baada ya fedha hizo kukusanywa na TRA. Tabia hii ya kupora Fedha za Mamlaka nyengine licha ya kwamba fedha hizo zimewekwa kisheria na kikatiba inaua misingi ya matumizi bora ya Fedha za Umma".

Akitoa mapendekezo ya nini cha kufanya Zitto ameeleza kwamba, "hazina ihakikishe inazirejesha kwa wenye ada, tozo na mapato hayo ambayo TRA ilikusanya kwa niaba ya Idara, Wakala na Taasisi nyingine.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad