ICC Yaonywa na Trump Kuchunguza Jinai za Kivita za Marekani na Israel

ICC Yaonywa na Trump Kuchunguza Jinai za Kivita za Marekani na Israel
Rais wa Marekani Donald Trump ameionya vikali Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) dhidi ya kuchunguza jinai za kivita za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Trump alitoa onyo muda mfupi baada ya majaji wa ICC kukataa ombi la Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC aliyetaka kuchunguzwa jinai za kivita zilizofanywa na wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.

Trump sambamba na kupongeza uamuzi huo wa majaji hao wa ICC na kusema kuwa ni 'ushindi mkubwa wa kimataifa', amesisitiza kuwa Marekani na Israel zinapaswa kupewa kinga ya kutoshtakiwa na ICC.

Amesema, "Jitihada yoyote ya kuwashtaki Wamarekani, Waisraeli na waitifaki wake, itakabiliwa na jibu kali."

Haya yanajiri siku chache baada ya Marekani kubatilisha viza ya kuingia nchini humo Fatou Bensouda, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutokana na uchunguzi wake kuhusiana na utendaji wa vikosi vya Marekani huko nchini Afghanistan.


Kadhalika Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amenukuliwa akisema kuwa, Washington imejiandaa kuchukua hatua zaidi vikiwemo vikwazo iwapo Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC haitabadilisha mwenendo wake.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC Bi Fatou Bensouda alikuwa akisafiri mara kwa mara kuelekea New York Marekani kwa shabaha ya kufanya mazungumzo na maafisa wa Umoja wa Maraifa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wake wa jinai zinazodhaniwa kufanywa na wanajeshi wa Marekani huko nchini Afghanistan.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad