IGP Simon Sirro amewaonya wale wote watakaoandamana bila ya kuwa na kibali, kwani kwakufanya hivyo watakuwa wameingia kwenye uhalifu.
”Kuhusu maandamano nimeshatoa maelekezo, kama maandamano ni halali sina shida,”
”Lakini kama maandamano sio halali, shida ipo na inakuwa ni shida kwa yule atakaye andamana.”
”Kwa sababu kama unaandamana maandamano sio ya halali ni uhalifu na utapambana na polisi, kama ni halali taratibu zipo kama barua ipo na mmekubaliana kwamba unaendelea na tutakulinda hamna shida.”
”Lakini kama hujaleta barua ya kutupa taarifa kuwa utafanya maandamano na ukafanya unaingia kwenye uhalifu.”
”Niwaombe si wakati wa kutaka kujiingiza kwenye uhalifu pasipokuwa na sababu, fuata taratibu, mwishowe utaona jeshi la polisi baya wakati ni lakwenu, haskari hawa ni wakenu, ukienda Kigoma, Kagera, Geita ndiyo utaona jinsi gani askari wanafamnya kazi.”
Sirro ametoa onyo hilo wakati kukiwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kufanyika kwa maandamano ya mkoani Dodoma