Bashir atashtakiwa katika mfumo wetu wa mahakama," Lt Jen Omar Zain al-Abidin amewaambia wandishi habari
Hatutowavumilia wale wanaowaua raia," amesema.
Ameongeza kwamba hakuna raia wa Sudana atakayesafirishwa kwenda kujibu mashtaka katika nchi ya nje ilimradi baraza la jeshi lipo uongozini, lakini ameongeza huenda serikali ijayo ya kiraia ikaamua kulishughulikia hilo kwa njia tofauti.
Bashir anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu katika mzozo wa Darfur magharibi mwa nchi hiyo.
Mzozo huo ulianza mnamo 2003 baada ya waasi kujihami kwa silaha wakiituhumu serikali kwa kuwanyanyasa watu wa kutoka eneo hilo.
Maelfu ya watu waliuawa katika mzozo huo
Jeshi la Sudan: 'Omar al-Bashir Atashtakiwa Sudan na sio ICC'
0
April 12, 2019
Tags