Kajala Afichua Siri Safari Zake Za Dubai

Kajala Afichua Siri Safari Zake Za Dubai
DAR ES SALAAM: STAA ‘grade one’ kwenye filamu Bongo, Kajala Masanja amefichua siri ya safari zake Dubai kwa kusema kikubwa kinachomfanya aende kila baada ya mwezi si starehe bali ni sehemu ya kazi.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Kajala alisema kuwa watu wengi wanajiuliza sana anapata wapi hela za kutanua na kwenda huko kula bata lakini ukweli ni kwamba hiyo ni moja ya kazi yake anayofanya.

“Unajua mwingine anaweza kusema nakula bata tu lakini kula bata huko nimechagua kufanya kazi za kibalozi kwa nguvu huku uigizaji nikifanya kama kitu tu ninachokipenda na siyo cha kutegemea ndiyo maana watu wengi wanajiuliza. Pia siyo Dubai tu huwa naenda nchi nyingi tofauti,” alisema Kajala.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad