Usemi wa mchekeshaji Pierre Likwidi 'utabaki kuwa juu, 'juu kileleni', umeibuka Bungeni wakati wa vikao vya bajeti ambavyo vimeanza Jijini Dodoma. Leo kikao kilianza kwa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara ya Maji ambapo Naibu Waziri, Juma Aweso alitumia usemi maarufu wa Pierre
Likwidi wakati akijibu swali.
Majibu ya Naibu Waziri yalitokana na swali lililoulizwa na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje ambaye alihoji ya kutokamilika kwa miradi ya maji kwenye baadhi ya miradi katika jimbo lake.
"Kwa kuwa miradi mingi ya maji imesimamama kwenye Wilaya ya Mpwapwa na Kongwa hivi sasa wananchi wanakosa maji, kwa sababu wakandarasi hawajalipwa ni lini wakandanarasi watalipwa ili wananchi wapate maji", ameuliza lubeleje.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Juma Aweso amesema kwa sasa serikali iko mbioni kuhakikisha wakandarasi wanalipwa.
"Ni kweli tulikuwa na wakandarasi zaidi ya milioni 100.5 lakini tumeona wakandarasi wanaopaswa kulipwa, nimhakikishie kama ana certifacte yake, haijalipwa aniambie nimlipe na baada ya kumlipa nimwambie atabaki kuwa juu, juu kileleni".
Hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii kuliibuka sintofahamu juu ya kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda juu ya kupewa kipaumbele kwa baadhi y watu ambao wamekuwa hawana umuhimu kwenye jamii.