Kesi ya Mpemba wa Magufuli’ Kisutu kupewa Mamlaka ya Mahakama ya Mafisadi

Upelelezi wa kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Yusuf Ali maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli’ na wenzake watano umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Yusuf na wenzake watano, wanakabiliwa na mashtaka manne, likiwemo la kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Milioni 785.6 ambapo shauri hilo lipo mahakamani hapo tangu mwaka 2016.

Hatua ya kukamilika kwa upelelezi huo imeelezwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Wakili Nchimbi ameeleza kuwa wanatarajia kuipa mamlaka Mahakama ya Kisutu ianze kusikiliza kesi hiyo ambayo ilipaswa kusikilizwa Mahakama ya ‘Mafisadi’.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba alikubaliana na hoja hiyo na kuahirisha kesi hiyo hadi Aprili 18, 2019 na washtakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu mashtaka yao hayana dhamana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad