Kijana Aliesaidiwa na Wabunge na Wananchi ili Apate Matibabu Afariki Dunia
0
April 28, 2019
Kijana aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la mguu wake wa kulia kuvimba pasipo kawaida amefariki dunia jioni jana akiwa chini ya uangalizi wa Madaktari hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara Ester Mahawe aliekuwa anafuatilia taarifa za mtoto Josephat Shabani, alitoa taarifa za kifo hicho ikieleza ’Mtoto Josephat amefariki dunia jioni hii Muhimbili,madaktari wamesema ile ilikuwa ni kansa na ilishafika mbali,Imeniuma sana jamani. Ila Mungu awabariki tumefanya sehemu yetu”. Aliandika Ester Mahawe kwenye mtandao wa kijamii wa Whatsap.
Taarifa iliyotolewa leo april 28 na mchungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima George Bilingi aliekuwa akifuatilia kila hatua hali ya mtoto huyo, imeeleza kuwa Mwili wake umehifadhiwa hospitalini hapo.
Mama wa mtoto huyo hakuwa na uwezo kifedha jambo ambalo lilimfanya mchungaji George kupost video fupi kwenye mitandao ya kijamii huku akiambatanisha namba ya simu ili mwenye kuguswa aweze kumsaidia.
Hata hivyo jitihada za Mchungaji huyo anaetoa huduma katika kanisa la Ufufuo na Uzima tawil la Babati Mjini, zilizaa matunda ambapo wabunge na watu wengine waliguswa na kumchangia kijana huyo zoezi likiongozwa na Mbunge Ester Mahawe na Anna Gidarya ambapo walifanikiwa kukusanya Shilingi Milioni 1,936,500.
Wabunge wengine waliojaribu kuokoa maisha ya Josephat Shabani kwa kutoa michango yao ni Jituson,Flatery Masai,Zacharia Isaay na Paulina Gekul .
Josephat Shabani alipata tatizo akiwa anafanya kazi kwa mtu kama kibarua kuchimba kisima ndipo alipojikwaa na baadae kushindwa kutembea baada ya goti kuteguka na baada ya hapo hali ikabadilika na kupelekea mguu wake kuumuka pasipo kawaida.
Kijana huyo alipelekwa hospitali huku serikali kupitia kwa waziri wa afya Ummy Mwalimu ikisema kuwa ingemtibu bure kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa awali na Mbunge Ester Mahawe na Paulina Gekul wa jimbo la Babati mjini baada ya kufanya mazungumzo.
Tags