Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais wa Urusi Vladmir Putin watakutana Alhamisi katika mji wa bandari wa Vladivostok kuujadili mkwamo wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Mshauri wa siasa za kimataifa katika Ikulu ya Urusi Yuri Ushakov amewaambia wanahabari katika miezi michache iliyopita hali katika rasi ya Korea imetulia, kwa kiasi kikubwa kutokana na juhudi za Korea Kaskazini za kusitisha majaribio ya makombora na kufunga kituo chake cha kufanyia majiribo ya nyuklia.
Kwa hiyo Urusi inataka kusaidia kwa njia yoyote ile kuyaendeleza mafanikio hayo.
Wachambuzi wanasema ziara ya Kim nchini Urusi ni ya kutafuta uungwaji mkono wa mataifa ya kigeni, baada ya kuvunjika kwa mkutano wa pili wa kilele kati ya Marekani na Korea Kaskazini mjini Hanoi Februari mwaka huu.
Kim Jong Un na Rais wa Urusi Vladmir Putin Kukutana Kesho Alhamisi
0
April 24, 2019
Tags