Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera ameeleza kuwa haridhishwi na mwenendo wa ratiba pamoja na uendeshaji wa ligi kutokana na klabu ya Simba kubakiwa na viporo 11.
Zahera ameamua kufunguka tena kutokana na mechi nyingi ambazo Simba wamebaki nazo msimu huu wakati timu zingine zikiwa na michezo michache.
Ameeleza kwa kuwataka TFF na Bodi ya Ligi kupanga ratiba kwa umakini bila kuonesha upendeleo wowote kwa timu zingine jambo ambalo kama yeye halifurahii.
Katika ratiba mpaka sasa inaonesha Simba amesaliwa na mechi takribani 16 ili kumaliza ligi msimu huu lakini kuna baadhi zimebakiza mechi 5.
Zahera pia amesema kuna upendeleo kwa namna moja ama nyingine unafanyika kutokana na timu yake kupangiwa mechi nyingi mfululizo ambazo zinafanya wachezaji wake wapatwe na wakati mgumu.
Zahera amedai wingi wa viporo hivyo kwa Simba inaondoa ushindani wa soka kwenye ligi kwa sababu wengine wamebakiza mechi 5, 6, 7, 8 huku Simba wakiwa wamebakiza mechi 16 kumaliza ligi.