Kongamano la Msanii Kujitambua Laandaliwa na Bodi ya Filamu

BODI ya Filamu Tanzania imeandaa kongamano Aprili 9 mwaka huu, litakalowajumuisha waigizaji, watayarishaji na wadau kwa lengo la kuwajengea uwezo katika sekta ya hiyo ili  kujitambua, kujithathmini na kujitangaza.



Akizungumza na Global Publishers Ltd, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Joyce Fissoo, amesema kongamano hilo litafanyika Aprili 15 katika ukumbi wa Suma JKT Mwenge.



“Kongamano hili litaanza mida ya saa 2 asubuhi hadi 12 jioni na kuwakutanisha wadau wote wa maigizo,  watayarishaji na viongozi wa kidini ili kusaidia umuhimu wa msanii kujua haki zake  na pia mikataba.



Aidha amesema mada watakazozizungumzia ni kuhusiana na namna ya utawala unavyojitangaza na pia kumfundisha msanii nidhamu ya kutumia fedha wakati anapozitapa.



“Wasanii wanapata fedha nyingi kutokana na kazi yao lakini hawana nidhamu ya fedha na huenda  ndiyo maana  utakuta msanii anashindwa kumiliki hata nyumba.  Kwa hiyo katika kongamano hilo tutapata maelekezo  ya namna ya kuwa na nidhamu na fedha,” alimalizia Joyce.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad