Korea Kaskazini imesema kuwa imefanyia majaribio silaha yenye kombora kali , ikiwa ni mara ya kwanza tangu mazungumzo kati ya rais Donald Trump na Kim Jong un kugonga mwamba.
Vyombo vya habari vya serikali vilitoa maelezo , lakini wachanganuzi wanansema kuwa jaribio hilo halionekani kuwa lile la kombora la masafa marefu ambalo ni tishio kwa Marekani.
Jaribio jingine kama hilo mnamo mwezi Novemba lilionekana kama hatua ya kuishinikiza Marekani kurudi katika meza ya mazungumzo.
Kumekuwa na hatua chache zilizopigwa tangu mazungumzo ya kinyuklia yaanze msimu wa joto uliopita.
Mnamo mwezi Februari , Donald Trump na Kim Jong Un walikutana katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi kuzungumzia usitihswaji wa umiliki wa silaha za kinyuklia , lakini mazungumzo yalivunjika huku viongozi wote wawili wakiondoka ghafla.
Wiki iliopita bwana Kim alisema kuwa rais Trump alifaa kuwa na tabia nzuri ili ,mazungumzo kuendelea.
KCNA iliripoti kwamba jaribio hilo lilifanywa katika awamu kadhaa za kulirusha , ambapo wachanganuzi wanaamini huenda silaha hiyo ilijaribiwa kutoka katika ardhi, baharini ama angani.
Bwana Kim alisema kuwa hatua hiyo ilikuwa na uzito mkubwa katika kuimarisha jeshi lake.
Ripoti hiyo ilitoa maelezo machache hivyobasi haijulikani iwapo lilikuwa kombora , lakini wadadisi wanasema kuwa huenda ilikuwa silha ya masafa mafupi.
Mwaka uliopita , kiongozi huyo wa Korea alisema kuwa atasitisha majaribio ya silaha za kinyuklia na kwamba hatofanyia majaribio makombora ya masafa marefu huku uwezo wa Kinyuklia wa Pyonyang ukibainika.
Vitendo vya kinyuklia vilionekana vikiendelea, hatahivyo picha za Setlaiti katika kiwanda kikubwa cha kinyuklia cha taifa hilo wiki ilioipita zilionyesha kulikuwa na vitendo vilivyokuwa vikifanyika-zikidai kwamba huenda Korea kaskazini inatengeneza mionzi kuwa mafuta ya bomu.
Taifa hilo linadai kwamba limetenegeza bomu la kinyuklia ambalo linaweza kuingia katika kichwa cha silaha ya masafa marefu pamoja na kombora ambalo linaweza kufika Marekani,
Mchanganuzi wa Korea Kaskazini Ankit Panda alisema kwamba tangazo hilo la mwisho lilifuatia zoezi la kijeshi lililofanyika kati ya Marekani na Korea kusini na kusema kuwa jaribio hilo lilipanga kulipza kisasi.
Korea Kaskazini Imelifanyia Majaribio Kombora Lake Jipya
0
April 18, 2019
Tags