Kuanguka kwa Gor Mahia kwaipa mteremko Tanzania

Kuanguka kwa Gor Mahia kwaipa mteremko Tanzania
Kufuatia kufanya vizuri msimu huu katika michuano ya Klabu Bingwa Africa, klabu ya Simba imeipatia Tanzania nafasi nne za kushiriki michuano ya vilabu inayoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika msimu wa mwaka 2020.


Simba imefikia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kabla ya kuondolewa na TP Mazembe, ambapo imefikisha jumla ya pointi 18 na kuisaidia Tanzania kupanda hadi nafasi ya 12 ya ubora wa vilabu barani Afrika. Pointi tatu kati ya hizo 18 zikitokana na Yanga kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho katika mwaka 2016 na 2018.

Gor Mahia ya Kenya ambayo ilikuwa ikishiriki michuano ya Shirikisho barani Afrika, imeondolewa na klabu ya RSB Berkane ya Morocco na hivyo kushindwa kuongeza pointi zaidi baada ya kuwa na pointi 14 kwenye hatua hiyo iliyoishia.

Kwanini Tanzania inapeleka timu nne 2020 na sio 2019?


Kanuni zinasema kuwa nchi itakayofikia pointi 12 katika msimu wa michuano ya vilabu barani Afrika, baada ya misismu miwili itapata nafasi ya kuingiza klabu nne katika michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF.

Endapo Gor Mahia ingeshinda mechi yake ya robo fainali na kufuzu hatua ya nusu fainali, ingeipokonya Tanzania nafasi ya kupeleka timu nne katika michuano hiyo. Kwa maana hiyo sasa, Tanzania itapeleka timu mbili katika Klabu Bingwa Afrika na timu mbili katika Kombe la Shirikisho katika msimu wa 2020/2021.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad