Kundi la Kiislamu la Thowheed Jamaath Ladaiwa Kuhusika na Shambulio la Makanisa Sri Lanka

Sri lanka iko kwenye siku ya maombolezo kwa ajili ya watu 290 waliopoteza maisha. Mazishi ya watu wengi waliouawa kwa mashambulizi ya mabomu siku ya sikuu ya Pasaka watazikwa.

Polisi walipata vilipuzi zaidi siku ya Jumatatu na moja ya vilipuzi kililipuka hapo hapo wakati wataalamu walipokua wakijaribu kutegua bomu.

Changamoto iliyopo sasa ni kwa vyombo vya usalama kurudisha hali ya kujiamini miongoni mwa wananchi.

Kwa Picha: Shambulio la makanisa Sri Lanka
Baada ya mashambulizi, serikali ilitangaza hali ya dharura kuanzia usiku wa Jumatatu, hatua ambayo itawasaidia kuvipa nguvu vyombo vya ulinzi na usalama, kuwakamata na kuwahoji washukiwa bila amri ya mahakama.

Serikali ya Sri Lanka imesema kundi la kiislamu lenye msimamo mkali la Thowheed Jamaath, limehusika na mashambulizi ya mabomu. Lakini haijawekwa wazi kama kweli kundi hilo limehusika.

Sri Lanka ilikumbwa na mashambulizi ya namna hiyo, mashambulizi ya kujitoa muhanga yalikua yakitelekezwa na waasi wa Tamil Tiger wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.Lakini madhara ya liyojitokeza sasa yameshtua mno kutokana na idadi ya watu waliopoteza maisha kuwa kubwa.

Mashambulizi haya yameacha kidonda katika taifa hilo, kidonda kitakachochukua muda mrefu kupona.

Katika hatua nyingine Ubalozi wa China nchini Sri Lanka leo imewaonya raia wa China kutoingia nchini Sri Lanka siku za hivi karibuni .China ni Mwekezaji mkubwa zaidi nchini Sri Lanka.

Ubalozi umesema itakua vigumu kwake kuhakikishia usalama raia wa china kipindi hiki

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad