Lulu Diva Atuhumiwa Wizi

Lulu Diva atuhumiwa wizi
Msanii wa kiume wa Bongo Fleva, Ferouz, amemtuhumu Lulu Diva kuwahi kumuibia pesa wakati akimuuzia duka lake, na kununua fenicha za ndani.

Akizungumzia hilo, Ferouz amesema kwamba alimuajiri Lulu Diva kumuuzia duka lake wakati bado hajapata umarufu, lakini msanii huyo alikuwa akimuibia pesa nyingi hadi kufikia hatua ya kwenda kumshtaki polisi.

“Alikuwa aniniibia hela kibao dukani, anasema ametoka Tandale amehamia Mwananyanla, mimi ndio nimemuhamishia Mwananyamala kwa pesa zangu za duka langu, baada ya kuiibia, nikakuta amejaza mafenicha, ma Tv, ma sofa, kupitia pesa zangu, lakini anasahau ni kitu gani kimemsogeza hapo alipofika, na mimi ndio nimesababisha, hata hizo hela alizosema nilikuwa simlipi alikuwa anaiba, hadi kesi zipo pale polisi mabatini, hicho kitu kiko wazi”, amesema Ferouz.

Hata hivyo Ferouz amesema kwamba msanii huyo hakuwa sahihi aliposema kuwa hakuwa akimlipa alipokuwa anamfanyia kazi, na kama ni kiki kwa ajili ya wimbo wake basi asifanye muziki wa kiki ili apande.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad