Makamu wa kwanza wa Rais (Mstaafu) wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hawajarudisha kadi ya chama chake cha zamani cha CUF, lakini wameweka utaratibu maalumu wa kuirudisha yeye na wenzake.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Aprili mosi, 2019 wakati wa mahojiano katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds TV.
“Tumeshadhamiria wote kila aliyekuwa mwanachama wa CUF bendera zote, Katiba, sare na kadi tunazikusanya na kumkabidhi kiongozi wa chama (Zitto Kabwe) azikabidhi kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye atajua cha kufanya,” amesema Maalim Seif.
Mbali na hilo, Maalim Seif amesema uamuzi wake wa kujiunga ACT- Wazalendo haujamshusha umaarufu wake bali upo palepale.
1.Nakumbuka wakati tunatia saini muafaka wa Zanzibar Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjamini Mkapa alisema hakuna mwenye hatimiliki ya Tanzania kwahiyo sote tuna haki sawa juu nchi hii.
2.Rai yangu kwa Watanzania nawaomba tuungane kwa pamoja kwa ajili ya nchi yetu. Hakuna mwenye hatimiliki ya nchi hii ni mali ya wananchi wote kwahiyo wananchi wasiogope pale tunapoipinga CCM tuna mawazo mbadala juu ya nchi hii.
3.Watawala waliona kuninyang’anya CUF watanimaliza na mimi ntajiunga Chadema bahati mbaya hesabu zao zilikuwa wrong nikajiunga na ACT Wazalendo.
4.Mara ya mwisho kuzungumza na Rais Shein ilikuwa Machi 2016 mpaka sasa huwa tunakutana kwenye shughuli na wala hatuzungumzi hata kidogo. Na walinzi wake wakijua naenda mahali hupigiana simu na kuwaambia wanieke mbali naye.
5.Majengo yaliyokuwa mali ya CUF ni Mtendeni na Kilimahewa majengo yaliyobakia yalikuwa majengo ya wanachama Sasa kama wameamua kuondoka na kujiunga na ACT hawawezi kuyaacha CUF kwa mapenzi yao wameyarudisha ACT Wazalendo.
6.Wale waliochoma Bendera walikuwa tu na hasira na wala sikuunga mkono jambo lile, Jukumu letu na Mhe. zitto Kabwe ni kuwasihi vijana kuwa watulivu .
7.Mimi sina chuki na mtu, nikikutana na msajili nitamsalimu vizuri tu na nitamwambia ajitathmini kama je anatenda haki?
8.Mimi nilikuwa accounting officer wa Chama msajili alipoanza kutoa Fedha za ruzuku kwa Upande wa Lipumba nikamuandikia barua msajili kuhusu uamuzi wa kutoa pesa kwa Lipumba na mimi sijui si sawa basi mimi nikajivua nafasi hiyo.
9.Kwa ninavyomjua msajili wa vyama vya siasa, kama ningesema naanzisha chama changu asingenipa usajili. Msajili huyu kamrejesha Lipumba, amekata ruzuku akisema eti tuna mgogoro lakini kumbe alikuwa anampa Lipumba ruzuku hiyo tena kwa akaunti isiyo ya taifa
10.Hata kama ningeanzisha Chama changu msajili asingenipa usajili, Sikuona sababu ya kuanza upya kama kuna Alternative ya kuendeleza harakati. Maana wakati wa mgogoro wetu na Lipumba alikuwa anampatia pesa za ruzuku Lipumba .
11.Mimi umaarufu ninao tangu nipo CCM. Mimi sikutoka CCM nilifukuzwa, tena nilifukuzwa wakati mbaya sana sababu hapakuwa na chama kingine. Kuna watu wanasema wanafuatwa na CCM na pesa lakini mimi na umri wangu huu tangu nimetoka sijawahi kufuatwa na eti nirudi CCM.
12.Wakati nikiwa CUF nimetengeneza kina Maalim Seif wengi sana na ndio maana nilikuwa naweza kuondoka nchini kwa hata miezi 6 na mambo yanakwenda, washauri wangu walikuwa wanakuja kwangu kwa ushauri tu”
13.Mimi binafsi nilisema nahama CUF nakwenda ACT Wazalendo nawaomba wanachama na wao waniunge mkono, sikuwaambia kuwa tunahama sote, wanachama kwenda ACT ni hiari yao, lakini wanachama wa CUF hasa wa visiwani walikuwa wamechoshwa na mgogoro
14.Tumekwenda ACT-Wazalendo sio kutafuta vyeo, bali kuongeza nguvu lakini ikitokea wametutunuku vyeo basi tutavipokea. ACT wana utamaduni wao ni kazi kwetu kujibadilisha ili kuendana nao
15.ACT wazalendo ina viongozi vijana wenye nguvu, uongozi wenye malengo ambao wakishaamua jambo wanafanya na kubwa zaidi dhamira yao kwa nchi yetu ni nzuri
Maalim Seif Afunguka Kuhusu Kurudisha Kadi Yake ya CUF, Umaarufdu Wake na Mambo Mengine. Tazama Hapa
0
April 01, 2019
Tags