Kumetokea mabishano ya kisheria baina ya mawakili wa upande wa utetezi na mashtaka kuhusu kupokea ungamo la mshtakiwa Hamis Chacha ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya mwanafunzi Humphrey Makundi wa shule ya Sekondari Scolaatica.
Mabishano hayo yalijitokeza wakati shahidi wa 14 wa upande wa mashtaka Irene Mushi ambaye ni Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Moshi na ni mlinzi wa amani alipoiomba Mahakama kupokea maelezo ya ungamo la mshatakiwa kama kielelezo mahakamani.
Shahidi huyo ameiambia Mahakama November 20.2017 Inspecta Tenga alimleta mtuhumiwa Hamis Chacha mbele yake anayetuhumiwa kwa mauaji hivyo anahitaji kuandika maelezo yake ambapo mlinzi huyo wa amani alimuamuru Inspecta atoke nje nakubaki na mhudumu wa mahakama na baadaye alibaki na mshtakiwa nakujitambulisha kwa mtuhumiwa kuwa yeye ni mlinzi wa amani.
Ameeleza alipomuuliza kuhusu maelezo aliyoandika Kituo cha Polisi kama ameshurutishwa, kulazimishwa nakusema ameandika kwa hiari yake.
Ameendelea kusema baada yakutoa maelezo hayo alimwambia haki zake za msingi kama amelazimishwa au ameshurutishwa nakusema alipomuuliza kuhusu maelezo yake kutumika kama ushahidi mahakamani alijibu yupo tayari yatumike.
Upande wa utetezi umeonyesha kupinga mahakama kupokea kielelezo alichokitoa shahidi wa 14 ambaye ni hakimu kwa kuwa kina mapungufu ya kisheria huku sababu ya pili hakikukidhi masharti ya uhiari.
Upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili David Shilatu baada ya mapingamizi yaliyowekwa na utetezi aliiomba mahakama kusikiliza sababu hizo za kisheria ili mahakama iweze kupima.
David Shiratu anayemtetea mtuhumiwa wa mauaji ya mwanafunzi Hamis Chache amesema hakuna sehemu ilipoonyesha muda uliopelekwa mbele yake pamoja na kutoulizwa na mlinzi wa amani alipolala mtuhumiwa nakusema maelezo hayo yanakosa sifa nakupinga kupokelewa.
Upande wa mashtaka kupitia kwa wakili Joseph Pande amesema hoja zilizotolewa na mawakili wa utetezi hazina msingi wowote nakuiomba mahakama kuzitupilia mbali na kwamba nyaraka inayobishaniwa imefuata misingi yote ya kisheria na inahaki yakupokelewa kama ilivyo
Ameongeza kwamba nyaraka yote ikisomwa eneo la muda wakukamatwa mtuhumiwa na alipolala na alitokea wapi kwenda kwa mlinzi wa amani vitu vyote vipo na hawakutaja kifungu chochote cha kisheria kwenye madai yao.
Kesi hiyo imengia katika hatua ya kesi ndani ya kesi ambapo imesikilizwa hadi saa moja na dakika 40 usiku katika mahakama kuu kanda ya moshi na jaji Frimin Matogolo na itaendelea leo April 11.