Taarifa tunazopokea ni kwamba madaktari wawili wa Cuba nchini Kenya wametekwa nyara na washukiwa wa kundi la Alshabaab katika mji wa Mandera.
Inaarifiwa kwamba mkasa huo umetokea mapema leo asubuhi wakati madaktari hao wakielekea kazini katika mji huo uliopo katika eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya.
Mwandishi wa BBC katika eneo hilo la Mandera Bashkas Jugosdaay anasema walinzi wa madaktari hao wameuawa na washambuliaji wamefanikiwa kutoroka kwa kutumia gari aina ya Probox.
Inaarifiwa madaktari hao wanaishi karibu na makaazi ya gavana wa eneo hilo ambayo ni kilomita takriban 4 kutoka eneo la mpaka na Somalia. l
Haijulikani ni washambuliaji wangapi waliokuwa ndani ya gari hilo aina ya Probox ambalo kwa mujibu wa duru lilikuwa limeegeshwa nje ya makaazi hayo.
Milio ya risasi imesikika katika mji wenyewe wa Mandera na kwa sasa maafisa wausalama wanawasaka watekaji hao.
Madaktari kutoka Cuba wafika Kenya kufanya kazi
Madaktari hao nimiongoni mwa wengine Kundi la la madaktari kutoka Cuba waliowasili Kenya kwa ombi la serikali kuja kupunguza uhaba wa madaktari nchini humo.
Miongoni mwa madaktari walio kwenye kundi hilo kutoka Cuba ni wataalamu watano wa figo, wataalamu wa x-ray, wataalamu wa mifupa na maungio na wataalamu wa mfumo wa neva.
Wamekuwa wakitoa huduma na kushauriana na madaktari wengine katika maeneo tofauti nchini.
Madaktari wa Cuba Nchini Kenya Watekwa na Washukiwa wa Alshabaab
0
April 12, 2019
Tags