Magufuli Awavaa Wakulima wa Korosho Wanaodai Hawajaoipwa..... Amuagiza Mkuu was Wilaya Kuwachukulia Hatua

Magufuli Awavaa Wakulima wa Korosho Wanaodai Hawajaoipwa..... Amuagiza Mkuu was Wilaya Kuwachukulia Hatua
Rais John Magufuli amewajia juu wakulima wa korosho mkoani Mtwara wanaodanganya kuwa hawajalipwa fedha zao na serikali jambo ambalo si kweli na kumuamuru Mkuu wa Wilaya kuwachukulia hatua wadanganyifu wote.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 2, wakati akihutubia wananchi mkoani humo katika ziara ya siku tatu aliyoianza ambapo pia ameweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege na kuwataka wakulima wa korosho kuacha kutoa kisingizio cha kutolipwa fedha za korosho katika kila jambo.

“Wakulima 17,616 hawajalipwa wenye kilo 1,500 kwa sababu nyingi tu, wapo waliowekewa fedha kwenye benki unakuta akaunti aliyoitaja jina ni tofauti na lake wapo waliokuwa hawana akaunti wakazungumza ilipiwe kwenye akaunti ya shangazi sasa fedha ya serikali haiendi hivyo.

“Waliotoa maelezo na wakabadilisha wakafungua akaunti na kadhalika sasa ni karibu asilimia 98 hadi 99 na ninataka niwaambie orodha yao ninayo, kila wilaya, mkoa, kijiji, akaunti na jina alilolipwa na nitamuachia Mkuu wa Mkoa ili mshirikiane na Mkuu wa Wilaya ili muangalie hao waliolipwa,” amesema.

Aidha, amewataa wafanyabiashara wadogo wadogo kutumia vitambulisho walivyopewa ili wasisumbuliwe wakati wanafanya biashara.

“Itafika mahali wale ambao hawatakuwa na vitambulisho hawataruhusiwa kufanya biashara katika baadhi ya maeneo kwa hiyo tumieni fursa hiyo na mnapokuwa na vitambulisho hivyo hakuna kudaiwa na mtu yeyote,” amesema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad