WATU wanaosadikiwa ni majambazi, wamevamia nyumbani kwa beki wa Kimataifa wa timu ya Simba, Pascal Wawa na kukomba kila kitu zikiwemo pesa kiasi cha dola 1,500 sawa na Tsh milioni 3. 47, huku wakimuachia nguo tu.
Tukio hilo la kusikitisha limemkumba nyota huyo usiku wa kuamkia Jumatatu ya Aprili 8, 2019 nyumbani kwake maeneo ya Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Jumatano kwa masikitiko Wawa alisema kuwa watu hao kabla hawajaingia ndani waling’oa madirisha na kutumia sehemu hiyo kama mlango.
“Majambazi wameingia nyumbani kwangu kwa kung’oa madirisha na kuondoka na kila kitu ambacho kilikuwa ndani kama unavyyona fedha zangu dola 1,500 hazipo,” alisema Wawa.
Majambazi Wavamia Nyumba ya Wawa na Kukomba Kila Kitu
0
April 11, 2019
Tags