Hayo yamesemwa leo April 8 2019,Bungeni jiji ni Dodoma na Waziri wa nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais ,Muungano na Mazingira ,Mhe.Januari Makamba wakati akijibu swali la Mbunge Wa Kaliua Tabora Mhe.Magdalena Sakaya aliyehoji kwa kuwa Mifuko ya Plastiki imezagaa kila mahali hapa nchini,serikali ina mpango gani wa kupiga marufuku matumizi ya Mifuko hiyo.
Katika Majibu yake Mhe.Makamba amesema serikali ina mkakati wa kupiga marufuku matumizi hayo na huenda ikasitisha kuanzia Mwezi Julai Mosi, Mwaka huu pindi taratibu zitakapokamilika.
Hata hivyo,Mhe.Makamba amesema mbadala wa matumizi ya mifuko ya Plastiki upo na itaibua ajira nyingi kwa watanzania tofauti na ilvyo sasa mifuko ya plastiki imekuwa ikitolewa bure madukani pindi mtu anunuapo bidhaa.