Makonda Akutana na Wajane Kutatua Changamoto Zao


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo Aprili 4, 2019 amekutana na wajane katika ukumbi wa  Mlimani City jijini Dar es Salaam ili kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili, likiwemo suala la mirathi na kutoa elimu kwao kuhusu fedha ambazo ni asilimia nne zinazotengwa na kila manispaa kwa wanawake ili wajue kuwa fedha hizo zinawahusu.


Mwenyekiti  wa kamati maalum iliyoundwa na Makonda kushughulikia matatizo yanayohusu ukatili hasa dhidi ya  watoto, Alberto Msando, akikabidhi  ripoti  hiyo kwa mkuu huyo wa mkoa.


“Nawashukuru sana viongozi wote walioonyesha sapoti katika hili, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa wilaya kwa kulisimamia hili. Lakini pia NGO’s zote tisa zilizoungana nasi kwenye hili. Kwa niaba ya serikali na Mungu tunasema asante sana.

“Zaidi wa wajane 300 walifika ofisini mwaka jana kwetu kuwa wamedhulumiwa. Pia dada Happyness Kijo aliponialika kanisani kwake, nilikuta wajane wengi anaowahudumia akiwa ameambiwa na Mungu. Nami nikasema nina haja ya kusaidia wajane.

“Tunalolifanya ni kutengeneza mifumo ya kudumu kwa vizazi vijavyo ili hata Makonda au Magufuli asipokuwepo basi wajao wataishi kwa furaha. Tuko vizuri na hatutachoka au kuacha.

“Nimekuja hapa wazazi wangu kuwatia moyo, kusema na mioyo yenu. Na ndiyo maana nimekuja na watu sahihi kama viongozi wa dini, ili muweze kuacha kulia na kuwa na matumaini mapya katika familia zenu. Muache majonzi na muwe na furaha.

“Pia nimekuja kuangalia mfumo wa sheria kama una changamoto, ninafanya nini mimi kama sehemu ya serikali kuweza kuweka mambo sana. Wajane wa sasa na wa baadaye waishi vizuri na watoto wao.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad