Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaasa wanafunzi kuachana na mitandao ya kijamii badala yake kuzingatia masomo ili waweza kufikia malengo waliyojiwekea .
RC Makonda ameyazungumza hayo alipokuwa akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Mzimuni alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi yote iliyopo ndani ya Mkoa huo ambapo ametembelea shule hiyo kuona ujenzi wa madarasa 6, unaoendelea.
Amesema ili waweze kufanya vizuri katika masomo wanatakiwa kuweka juhudi, nidhamu pamoja na kuheshimu malengo yao waliojiwekea ambapo amewataka wanafunzi hao kufanya vizuri ili Rais Dkt. John Magufuli kuweza kujivunia kuzalisha wanafunzi bora katika nchi yake.
“Mnauwezo mkubwa sana wakufanya vizuri achaneni na tabia za kukaa kwenye mitandao ya kijamii wekeni bidii kwenye masomo ili mje kulisaidia taifa, kuna mambo matatu ukiwa nayo lazima utafanya vizuri unatakiwa kuwa na juhudi, nidhamu pamoja na malengo, malengo yako lazima yawe tofauti na Dunia” amesema RC Makonda.
Amesisistiza kuwa wanafunzi wengi wamekiwa wakifuatilia mambo ya dunia jambo linalopelekea kufanya vibaya katika masomo.
Makonda Awaonya Wanafunzi Wanaotumia Mitandaoni ya Kijamii
0
April 17, 2019
Tags