Mamia ya raia wa kigeni waishio Afrika Kusini wakesha nje ya vituo vya Polisi wakihofia mashambulizi dhidi yao

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Afrika Kusini ameitisha mkutano wa dharura na mabalozi kufuatia mashambulizi dhidi ya wageni mjini Durban. Mapema Jumatatu watu watatu walifariki kufuatia maandamano yanayolenga maduka, mengi ambayo yanamilikiwa na wageni.


Kwa mujibu wa BBC. Takriban watu 50 walitafuta hifadhi katika kituo kimoja cha polisi wakati kundi moja la vijana wa Afrika wasio na kazi walipowashinikiza kutoka katika majumba yao usiku.

Wageni wanalengwa na watu ambapo wanawashtumu kuchukua kazi zao.

Amesema kuwa ghasia hizo, ambazo zimekuwa zikiwalenga raia wa Malawi na raia wengi wa Afrika katika jimbo la Kwazulu Natal ni swala la kujutia hususan katika mkesha wa siku ya mwezi wa uhuru ambapo taifa hilo linaadhimisha miaka 25 tangu uchaguzi wa kidemokrasia nchini humo.

Wiki iliopita , makumi ya raia walilazimika kutoka katika nyumba zao na waandamanaji waliojawa na hasira ambao pia waliwaibia maduka yao.

Ramaphosa ashutumu ghasia hizo
Wakati huohuo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameshtumu ghasia za hivi karibuni za mashambulizi dhidi ya wageni na kutoa wito kwa taasisi za kiusalama kuwakamata wanaotekeleza vitendo hivyo.

Amesema kuwa ghasia hizo, ambazo zimekuwa zikiwalenga raia wa Malawi na raia wengi wa Afrika katika jimbo la Kwazulu Natal ni swala la kujutia hususan katika mkesha wa siku ya mwezi wa uhuru ambapo taifa hilo linaadhimisha miaka 25 tangu uchaguzi wa kidemokrasia nchini humo.

Wiki iliopita , makumi ya raia walilazimika kutoka katika nyumba zao na waandamanaji waliojawa na hasira ambao pia waliwaibia maduka yao.

”Leo uchumi wetu na faida za jamii yetu zinatokana biashara na uwekezaji kutoka kwa washirika wetu katika bara Afrika na wengi wanaishi hapa nchini Afrika Kusini ambapo wanachamngia pakubwa maenedeleo ya taifa hili. Maendeleo ya Afrika yanatokana na ongezeko la watuna mizigo kutoka eneo moja hadi jingine kati ya mataifa tofauti ili sote tuweze kufaidika.hatutakubali kuwawacha wahalifu kurudisha nyuma hatua zilizopigwa”.


Kulingana na Edgebert Mkoko ambaye ni raia wa Tanzania anayeishi katika jimbo la kwazulu natal hali sio shwari hususan miongoni mwa raia wa Zimbabwe, Malawi na Ethiopia ambao ndio wengi wanaotafuta maisha katika eneo hilo. Mkono anasema kuwa kuna baadhi ya watu wanaodaiwa kuuawa katika eneo hilo.

”Vurugu zilizotokea hapo awali zimeibuka tena na chanzo ni kwamba raia wa kigeni wanaoishi nchini humo wanachukua kazi za raia wa taifa hilo”’.

Anasema kuwa bado hakuna suluhu yoyote iliotolewa na serikali hatua ambayo imewafanya raia wengi wa kigeni kuamua kusalia majumbani.

Anaongezea kuwa hali ngumu kwa raia wengi wa kigeni kwa kuwa wanaishi pamoja na raia wa kipato cha chini.

Mkoko anasema kuwa siku mbili zilizopita raia wengi wa kigeni walijaa katika vituo vingi vya polisi katika mji wa Durban

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad