MANCHESTER City sasa washindwe wenyewe kutwaa ubingwa baada ya kuwanyuka wapinzani wao wa jadi, Manchester United mabao 2-0 kwenye mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Matokeo hayo yameiumiza Liverpool, ambayo ni mahasimu wa Manchester United kwani sasa wameshuka hadi nafasi ya pili ya msimamo wa ligi wakiwa na pointi 88 na kuzidiwa pointi moja na Manchester City, ambayo inaongoza ligi baada ya kufi kisha pointi 89 huku timu zote mbili zikiwa zimecheza mechi 35.
Hali hiyo sasa inaiweka katika nafasi nzuri ya ubingwa Manchester City kwani sasa ikishinda mechi tatu zilizobakia itajihakikishia ubingwa kwani itafi kisha pointi 98 ambazo haziwezi kufi kiwa na Liverpool.
Kwani Liverpool ikishinda mechi zake tatu zilizosalia itakusanya pointi 97 ambazo haziwezi kuwapa ubingwa. Liverpool inakabiliwa na kazi mbili, ambapo moja ni kushinda mechi zake zote tatu zilizobaki na wakati huo kuombea Manchester City iteleze kwenye mechi zake
Nayo Manchester United imezidi kuhatarisha nafasi yao ya kushika nafasi nne za juu za Ligi Kuu England ili kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu ujao. Manchester United imebaki katika nafasi ya sita ikiwa na pointi 64, ambapo ipo pointi mbili nyuma ya Arsenal iliyolala mabao 3-1 kwa Wolves. Nafasi ya nne kwa sasa inashikwa na Chelsea, ambayo ina pointi 67.
Tottenham Hotspur inayokamata nafasi ya tatu na pointi 70 na Chelsea zikishinda mechi zao zote tatu zilizosalia zina nafasi ya kujihakikishia kukamata nafasi zao. Manchester City, ambayo ilimiliki mpira zaidi katika mchezo wa jana, ilipata bao lake la kwanza mnamo dakika ya 54 likipachikwa na Bernardo Silva, ambaye alimbabaisha beki wa kushoto wa Manchester United, Luke Shaw kabla ya kupiga shuti la chini lililotinga wavuni.
Leroy Sane alifunga bao la pili la Manchester City baada ya kupiga shuti lililombabatiza kipa wa Manchester United, David de Gea kabla ya kutinga wavuni kufuatia pasi ya Raheem Sterling katika dakika ya 66.
Miamba hiyo ilikuwa ikicheza kwa staili tofauti jana, ambapo Manchester United walikuwa wanavizia kwa kufanya mashambulizi ya kushitukiza `counter attack’ huku Manchester City wakimiliki mpira zaidi na huku wakijenga mashambulizi yao kwa pasi fupi fupi.
Wakati huo huo, Arsenal iliididimiza matumaini yao kushika nafasi nne za juu za ligi baada ya kucharazwa mabao 3-1 na Wolverhampton Wanderers kwenye mechi nyingine ya ligi. Matokeo hayo yameifanya Arsenal kubakia kwenye nafasi ya tano ikiwa na pointi 66 wakati Wolves imeruka hadi nafasi ya saba baada ya kufi kisha pointi 51.