Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa sababu zinazolalamikiwa na klabu ya AS Vita kuwa walifanyiwa vurugu hazina ukweli wowote.
Manara amesema kuwa klabu zote zilizokuja kucheza Tanzania katika Klabu Bingwa Afrika zilitoa malalamiko ambayo hayana ukweli wowote na hata AS Vita na walifanya hivyo kwakuwa walishaidharau Simba na hawakutegemea kuwa watafungwa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amesemaa, "huu ni uongo mtakatifu, Soura walilalamikia media kwa kutotoa taarifa ya ukweli, Ahly hawakulalamikia chochote, AS Vita walilishwa matango pori na Zahera na wenzie na hawa washaanza uoga wao!", amesema Manara.
"Shida ya hivi vilabu vya Congo vinadhani vinayo haki ya kutufunga kila siku, wakifungwa wao misababu milioni, wakitufunga wao ni sawa!!. Guys hii kikwetu tunaita mchecheto na tuwaambie kabisa, Taifa ni mahali tulipokabidhiwa Uhuru wetu lazima tupaenzi kwa kutoa vipigo takatifu!! Hahahahaha, halafu why wanatumia picha yangu?. Haji anacheza namba ngapi? hihihihi naogopewa kama mimi ndio kagere?".
"Ila napaishwa sana na hivi vilabu vya nje. Na kwa hali hii siendi Congo, usalama wangu ushakuwa mdogo".
Simba na TP Mazembe zinatarajia kupambana katika Uwanja wa Taifa Dar es salaam, Jumamosi hii, April 6 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa klabu bingwa Afrika