Maporomoko Yaua Watu 60 Durban Afrika Kusini

MAPOROMOKO ya udongo yaliyotokana na mvua kubwa yamesababisha vifo vya watu 60 katika mikoa ya Durban na KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.



Zaidi ya watu 1,000 wameondoka kutoka makazi yao kwa mujibu wa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa,  ambaye ametembelea maeneo yaliyoathiriwa.



Mvua kubwa imekuwa ikinyesha katika maeneo ya kusini na mashariki mwa nchi hiyo siku chache zilizopita. Mafuriko zaidi na upepo mkali unatarajiwa katika maeneo ya pwani huku onyo likitolewa kuhusu hali mbaya ya hewa.



Mafuriko hayo makubwa yaliharibu biashara na nyumba za watu  na vyuo vikuu viwili – huku mamia ya watu wakiondoka katika makazi yao.






Ramaphosa amezitembelea familia zilizopoteza wapendwa wao katika mafuriko hayo. Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko amesema  kuwa rais aliweka shada la maua katika eneo ambalo watu wanane walifariki.



Pia alionekana akiwasukuma walinzi waliokuwa wakiwazuia watu kusema naye.

“Ni muhimu kuja kuona kile kilichofanyika au kilichotokea na kuomboleza na familia zilizopoteza wapendwa wao katika janga hili. Kupoteza maisha sio jambo rahisi, hasa maafa yakitokea ghafla,” alisema Ramaphosa.






Wakati hayo yakijiri, Waziri wa Tawala za Mikoa, Nomusa Dube-Ncube,  amewaambia maofisa wa kituo cha radio cha SAFM kwamba bado wanaendelea kutathmini kiwango cha uharibifu uliosababishwa na mkasa huo, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.



Siku zijazo watu watalazimika kuhamishwa kutoka maeneo yaliyoathirika, alisema. Watu kadhaa wamepelekwa hospitali huku shughuli ya kuwatafuta manusura waliyozikwa chini ya vifusi vya majengo yalioporomoka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad