Marekani yafutilia mbali visa ya muendesha mashtaka wa mahakama ya ICC Fatou Bensouda


Marekani imefutilia mbali Visa ya kuingia nchini humo ya kiongozi wa mashtaka wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita Fatou Bensouda.

Uamuzi huo unadaiwa kuwa jibu la uchunguzi wa Bensouda kuhusu uhalifu wa kivita uliotekelezwa na vikosi vya Marekani na washirika wake nchini Afghanistan.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani alikuwa ameonya kwamba Marekani inaweza kuwakataa ama kufutilia mbali Visa vya maafisa wowote wa ICC wanaohusishwa na uchunguzi huo.


Tajiri mkubwa duniani kulipa $35bn kwa talaka
Afisi ya Bensouda ilisema kuwa kiongozi huyo wa mashtaka ataendelea na jukumu lake bila kuogopa ama kupendelea upande wowote.

Waziri wa maswala ya kigeni Mike Pompeo alisema: Iwapo unahusika na pendekezo la ICC la kuwachunguza wanajeshi wa Marekani kuhusiana na hali ya Afghanistan , usidhani kwamba utaendelea kuwa na

visa ya Marekani ama kuingia nchini humo.

''Tumejiandaa kuchukua hatua zaidi ikiwemo vikwazo iwapo ICC haitabadilisha mwenendo wake'', aliongezea.

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image caption
Fatou Bensouda alianza kuwa muendesha mashtaka wa mahakama hiyo 2012
Ripoti ya 2016 kutoka mahakama ya ICC imesema kuwa kulikuwa na sababu muhimu kuamini kwamba jeshi la Marekani lilitekeleza mateso katika kituo kimoja cha siri nchini Afghanistan kinachoendeshwa na shirika la ujasusi la Marekani CIA na kwamba serikali ya Afghanistan na wapiganaji wa Taliban walitekeleza uhalifu wa kivita.

Marekani ambayo imekuwa ikiikosoa sana mahakama ya ICC tangu ilipoanzishwa ni miongoni mwa makumi ya mataifa yaliojiunga na mahakama hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad