Marekani imeweka vikwazo zaidi kuzilenga meli za kampuni ya mafuta ya Venezuela na kampuni nyingine zinazofanya biashara na mshirika wake muhimu Cuba.
Kwa kuweka vikwazo hivyo vipya Marekani inatumai kumfungia Rais Maduro njia muhimu kabisa za kibiashara.
Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence alitangaza hatua hizo mjini Washington ikiwa ni sehemu ya jitihada za Marekani za kutaka kumuondoa madrakani Rais Maduro.
Makamu wa Rais Pence pia amesema nchi yake inaazimia kuishinikiza zaidi Cuba. Cuba ni mnunuzi mkubwa wa mafuta ya Venezuela na pia inaunga mkono utawala wa Maduro.
Wakati huo huo mvutano kati ya Rais Maduro na kiongozi wa upinzani Juan Guaido unazidi kupamba moto.