Msemaji wa Wizara hiyo Robert Palladino ameitaka serikali nchini humo pia kuwaruhusu wanahabari wanaofanya kazi na mashirika hayo, kuwaacha kufanya kazi yao kwa uhuru kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.
Burundi imechukua hatua hiyo kwa madai kuwa mashirika hayo ya Kimataifa hayafuati sheria zinazotoa muongozo wa uandishi habari nchini' na 'kukiuka maadili ya kikazi'.sheria za nchi hiyo kuhusu uanahabari.
Inaishutumu BBC kwa kushindwa kumwajibisha mwanaharakati wa Burundi katika mahojiano aliyofanyiwa katika idhaa ya kifaransa ya shirika hilo.
Radio kadhaa za kibinafasi zimeharibiwa na kufungwa nchini humo wakati wa mzozo wa kisiasa ulizuka mnamo 2015, wakati rais Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais alioshinda baadaye.