Mashambulizi dhidi ya wageni Afrika Kusini: Serikali Kukutana na Mabalozi Pamoja na Maafisa wa Polisi

Mashambulizi dhidi ya wageni Afrika Kusini: Serikali kukutana na mabalozi pamoja na maafisa wa polisi
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Afrika Kusini ameitisha mkutano wa dharura na mabalozi kufuatia mashambulizi dhidi ya wageni mjini Durban.

Mapema Jumatatu watu watatu walifariki kufuatia maandamano yanayolenga maduka, mengi ambayo yanamilikiwa na wageni.

Takriban watu 50 walitafuta hifadhi katika kituo kimoja cha polisi wakati kundi moja la vijana wa Afrika wasio na kazi walipowashinikiza kutoka katika majumba yao usiku.



Takriban watu 100 walishambulia maduka ya vyakula siku ya Jumapili usiku na Jumatauj alfajiri , wakiiba na kuchoma majumba.

Mwanamke mmoja alifariki wakati alipoanguka kutoka kwa paa la nyumba wakati alipokuwa akiwatoroka waandamanaji hao.

Watu wengine wawili waliuawa kutokana na majeraha ya risasi , baada ya mwenye duka moja kudaiwa kuwapiga risasi.

Siku ya Jumanne wageni walianza kutafuta hifadhi katika misikiti na kituo cha polisi.

Waziri wa mahusiano ya kigeni na ushirikiano Lindiwe Sisulu aliwaagiza maafisa wa polisi kuwakabili watu wanaowashambulia wageni.

''Vitendo vyovyote vya kihuni pamoja na wizi wa mali ya raia wa kigeni hautakubalika na maafisa wa polisi na taasisi za kiusalama zinafaa kuchukua hatua za dharura bila kupendelea upande wowote'', alisema katika taarifa.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Ameandaa mkutano na wanadiplomasia wa Afrika.

Baadhi ya watu hulalamika kuhusu wageni wanaofanya kazi nchini Afrika Kusini ambapo ukosefu wa ajira uko juu ukiwa asilimia 72 mwisho wa mwaka uliopita.

Mashambulizi dhidi ya wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika sio jambo geni nchini Afrika kusini.

Mwaka 2015, ghasia katika miji ya Johannesburg na Durban zilisababisha mauaji ya watu saba baada ya wahamiaji kuwindwa na kushambuliawa na magenge.

Afrika kusini ilikumbwa na ghasia mbaya zaidi dhidi ya wageni mwaka 2008 wakati ambapo zaidi ya watu 60 waliuawa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad