MOTO umemuwakia Kocha msaidizi wa zamani wa Simba, Masoud Djuma baada ya kutimuliwa na AS Kigali kutokana na timu hiyo kuwa na mwenendo mbaya.
Djuma alipewa ukocha mkuu ndani ya kikosi cha AS Kigali, Oktoba mwaka jana na kudumu miezi sita pekee kabla hajatimuliwa ndani ya kikosi hicho.
Alitua hapo baada ya kufukuzwa Simba. Sababu kubwa iliyomuondoa Masoud katika nafasi ya ukocha wa timu hiyo ni matokeo mabaya waliyokuwa nayo timu hiyo sambamba na kupotea kwa nidhamu ndani ya kikosi.
Taarifa ya kutimuliwa kwa Masoud ilitolewa jana asubuhi na uongozi wa timu hiyo ambao umewapa timu Jean De Dieu na Nshutinamagara Ismael ‘Kodo’ hadi watakapopata kocha mpya. Chini ya Masoud, AS Kigali wamecheza mechi 23, wakishinda saba, wakifungwa saba na sare tisa.
Hawakashinda katika mechi zao tano mfululizo wakiwa na sare tatu na kufungwa mbili. Lakini habari za ndani zinasema AS Kigali hawafanyi vizuri kutokana na ukata na kikosi chao hakikuwa imara.
Masoud alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Simba lililotwaa ubingwa msimu uliopita akiwa Pierre Lechantre