Mbasha Alizwa na Bintiye, Asimulia vya Ndani

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha ameeleza namna ambavyo mtoto wake wa kike alivyomtoa machozi kwa kumtafuta na kumtaka waishi pamoja.

Mbasha amefunguka hayo ikiwa ni baada ya hivi karibuni kupata nafasi ya kuonana na mtoto wake Elizabeth ambaye kwa muda mrefu alikuwa akiishi na mama yake (Madam Flora)
zamani Flora Mbasha baada ya kupeana talaka.

"Mwanangu amenitafuta ametafuta numba yangu kwa muda mrefu, alipoipata akanipigia kwa simu ya mtu na akaniambia baba nataka kuja uliko tuishi wote mpaka machozi yalinitoka sikutegemea nilishagajikatia tamaaa nilimwachia Mungu. Mtoto akamtafuta baba aliko, Asante Mungu".

Hata hivyo, Mbasha amewahoji wanawake wanapokosea kutokana na kuwalisha sumu ya chuki watoto kuhusu wazazi wao.

"Wamama mnakwama wapi, Kweli nimejifunza kitu hata umlishe sumu mtoto kiasi gani kwamba baba yako mbaya baba yako hafai baba yako alikutekeleza jalalani na mengine mengi. Ila mtoto akikua akijitambua anamtafuta baba yake popote alipo".

Kwa muda mrefu Mbasha amekuwa akieleza namna ambavyo mzazi mwenzake amekuwa akimnyima haki ya kuonana na mwanae tangu mwaka 2014 walipokumbwa na mgogoro uliopelekea ndoa yao kuvunjika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad