Maftaha Nachuma (CUF) Mbunge wa Mtwara Mjini, ambaye ni Mbunge wa Mtwara Mjini ameitaka serikali isiwatumie askari polisi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika.
Amesema kwamba pamoja na kwamba polisi wanatakiwa kulinda amani, serikali imekuwa ikiwatumia kuharibu uchaguzi na kukipendelea Chama cha Mapinduzi (CCM) na hicho ni kinyume na sheria ya utawala bora ambayo inatambua mfumo wa vyama vingi nchini.
Nachuma pia ameitaka tume ya uchaguzi iwe huru wakati wa chaguzi za serikali za mitaa ili kila chama kishiriki kwa mujibu wa sheria.
Nae Mbunge wa Moshi Mjini,Jafar Michael (CHADEMA) amewalaumu wakuu wa mikoa na wilaya kutumia madaraka yao vibaya kwa kuwanyanyasa wapinzani.