Mbunge Sugu Aitwa na Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, leo April 25, 2019 amewasili jijini Mbeya tayari kwa kuanza ziara ya siku 8 mkoani humo.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songwe jijini humo, Rais alipokelewa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila pamoja na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi.

Hata hivyo Rais Magufuli katika moja ya maeneo aliyosimama kusalimia wananchi waliojitokeza barabarani alimuita Mh. Mbilinyi na kumshukuru kwa mapokezi huku akimtania kuwa anaonekana moyoni ni CCM.

''Ndugu zangu maendeleo hayana chama na kwa kutambua hilo, mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Sugu amekuja kunipokea hapa, hebu njoo hapa wakuone na unavyopendeza tu unaonekana ni CCM'', alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametokea nchini Malawi ambako alifanya ziara ya kikazi ya siku 2 iliyoanza jana April 24 na kumalizika leo April 25.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad