Shirikisho la Soka Barani Ulaya(UEFA) limemfungia mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain baada ya kuandika maneno ya dharau na kejeli kufuatia timu yake kutolewa na Manchester United katika mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya
Mbrazili huyo, aliweka bandiko katika ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii wa Instagram lenye kuonesha hasira baada ya Man. Utd kupata penati ndani ya dakika nne za nyongeza wakati shuti lililopigwa na Diogo Dalot lilipomgonga Presnel Kimpembe mkononi
-l
Marcus Rashford alitumia nafasi hiyo aliyopewa na Muamuzi Damir Skomina aliyetoa penati hiyo baada ya kujishauri kutumia mfumo wa uamuzi wa runinga(VAR), kufunga goli na kufanya Manchester United kufuzu kucheza hatua ya robo fainali
Neyma aliandika "Hii ni aibu, wameweka watu wanne wasiojua chochote kuhusu soka kutoa maamuzi baada ya kuangalia marudio ya tukio kupitia VAR. Hakukua na penati. Panawezaje kuwa na penati wakati mpira umempiga mgogoni!" Kisha akatuna