Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro (CHADEMA) amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha amualike Rais John Pombe Magufuli jijini Arusha ili akapokea Shukrani na pongezi badala ya malalamiko.
Meya Lazaro ametaja baadhi ya miradi ya mfano na mafanikio iliyofanywa na Serikali jijini Arusha na pia kuelezea ushirikiano kati yake na Mkuu wa Mkoa Mh. Mrisho Gambo.
"Naomba mkuu wa mkoa umlete Rais Arusha, namuona yuko Mtwara anapokea malalamiko, mwambie aje Arusha apokee shukrani, aone mabwawa ya maji yanavyojengwa, aone barabara za lami,vituo vya afya na hospital ya wilaya na leo imeanza chanjo," amesema Kalisti Lazaro.
Ameendelea kwa kusema, 'Kwa hiyo niwaambieni sisi tunahitaji kuishukuru serikali ya awamu ya tano, na mimi kama Meya wenu nimejipanga, kasi yangu na ya Mkuu wa Mkoa na ya Rais huko juu tunaenda sambamba,'.