Hali hiyo, imechangiwa na bidhaa zisizo za vyakula kama vile mavazi na viatu, kodi ya pango, mafuta ya taa, mkaa, kuni, huduma za afya, dizeli, chakula na vinywaji.
Hayo yamesemwa jana jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Sensa ya Takwimu za Kijamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei wa kipindi hicho.
Kwisegabo alitaja baadhi ya bidhaa hizo kuwa ni pamoja na mavazi na viatu(4.4%), kodi ya pango(4.7%), mafuta ya taa(1.8%), dizeli(8.3%), chakula na vinywaji kwenye migahawa(4.6%) na malazi kwenye mahoteli(5.7).
Hata hivyo alifafanua kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa machi mwaka huu umepungua hadi asilimia 0.1 kutoka asilimia 0.5 kwa mwaka ulioishia Februari mwaka huu.