Ombi lake limefuatia shambulizi la angani lililofanywa na vikosi vya kamanda Khalifa Haftar kwenye Uwanja wa ndege wa Mitiga mashariki mwa Mji Mkuu wa Tripoli.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa Guterres amezitaka pande hizo mbili zinazohasimiana zisitishe mapigano ili kuepusha kuzuka kwa mzozo mkubwa nchini humo, Shambulizi hilo la angani lilisababisha kufungwa kwa Uwanja huo pekee wa ndege ambao unafanya kazi mjini Tripoli wakati makabiliano yakipamba moto karibu na mji huo mkuu na maelfu ya watu kukimbia.
Haftar alianzisha wiki iliyopita operesheni ya kukamata Tripoli wakati Guterres alikuwa nchini Libya kushinikiza makubaliano ya kisiasa kuhusu kuandaliwa uchaguzi.