Mnyika ahoji ripoti ya CAG kutogawiwa kwa wabunge 

Mbunge wa Kibamba (CCM) John Mnyika amehoji ni kwanini Wabunge hawajagawiwa ripoti  ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kama kanuni za Bunge zinavyosema.

 Mnyika ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo Aprili 12, alipokuwa akiomba mwongozo wa Spika Utawala Bora ambapo amesema kwamba kitendo cha wabunge kutogawiwa ripoti hiyo hakiwezi kuungwa mkono na wabunge kwa kuwa kinakiuka kanuni za Bunge.

Hata hivyo, ombi hilo la Mnyika liligonga mwamba baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kusema ripoti hizo za CAG haziwezi kugawiwa kwa wabunge kama Mnyika anavyotaka kwa kuwa kanuni haziruhusu kufanya hivyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad