MO Salah Afunguka Kutoifungia Liverpool Magoli

MO Salah afunguka kutoifungia Liverpool magoli
Februari 9 mwaka huu dhidi ya Bournemouth, ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa Mo Salah kuifungia goli Liverpool.

Hiki ndio kipindi kirefu kwa Mo Salah kucheza bila kuifunga goli Liverpool. .
Baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Tottenham Mo Salah amesisitiza kuwa hajali hata kidogo kutokufunga kama timu yake inaondoka na ushindi.

Salah juzi alifanya kazi kubwa katika upatikanaji wa goli la ushindi ambapo mpira wa kichwa alioupiga katika dakika ya 90 ulifanya beki wa Spurs Toby Alderweireld kujifunga.

“Sijafunga kwa mechi chache na kuna wachezaji wenye magoli sawa na mimi na wanasema (huu) ndio msimu wao bora katika maisha yao” Salah alimwambia beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher katika kituo cha Televisheni cha Sky Sports. .
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad