Msanii Bonta Achukizwa na Jokate Kutomshirikisha Kampeni ya Tokomeza Ziro na Kutumia Jina na Wimbo Wake Bila Ruhusa


Msanii wa Hip Hop Bonta, amuomba DC Jokate kumpa heshima yake kwa kutumia neno Tokomeza Zero "Nilihitaji kuheshimiwa"

Ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram:

"From @bonta_maarifa  -  MNYONGE MNYONGENI HESHIMA YAKE MPENI !!!
toka mwaka huu 2019 umeanza nimekuwa nikifatilia kwa karibu uhamasishaji wa Mh DC wa Kisarawe juu ya uhamasishaji wa kuondoa kabisa Division 0 katika wilaya hiyo "TOKOMEZA ZERO" hususani kwa watoto wa kike!
binafsi napongeza juhudi hizo kwa 100%!! ikumbukwe kuwa Mimi ni kati ya wanamuziki wa chache wa utamaduni wa HIP HOP ambao kwa zaidi ya miongo 2 tumekuwa tukiandika tungo zetu zinazojikita kwenye matatizo ya jamii inayotuzunguka "UJINGA, MARADHI, UMASKINI " ambavyo vyote vipo chini ya mwamvuli wa  SIASA!! na kwa masikitiko makubwa miongo yote hii tumekuwa TUKIBEZWA na washika dau kuwa aina hii ya muziki haina maslahi ! nilikuwa sina tatizo kama Mh DC na timu yake wanatumia neno TOKOMEZA ZERO!! lakini kampeni hii imeenda mbali kiasi cha kutumia nyimbo yangu ya TOKOMEZA ZERO niliyomshirikisha Barakah the Prince bila mawasiliano yoyote! ikumbukwe Mh DC ni mshika dau mkubwa wa muziki huu na ana nyimbo alishatoa na ana marafiki wengi ambao ni wasanii wanaosemwa ni wakubwa wa kimataifa wanaopewa nafasi kubwaa kwenye hii tasnia na wanaoimba nyimbo nyingi za MAPENZI na ULEVI na kupelekea kuhamasisha hizo ZERO kuongezeka, kwanini hakuchukua 1 ya nyimbo zao kuendeshea kampeni hii? tujifunze kuacha kubeza tungo za kijamii na kuzinyima nafasi !
audio ya TOKOMEZA ZERO nilirecord kwa Q THE DON kwa gharama ya laki 1,Video nilishoot na Luca Swahili kwa laki 5 na mashahiri niliyotumia kichwa changu na peni ya sh 100! gharama hiyo ndogo Leo inatumika KUKOMBOA WASICHANA WA KISARAWE na TANZANIA nzima!  kimsingi sikuhitaji malipo yoyote ya pesa kwenye kampeni kama hii ya kijamii ! niliitaji kuheshimiwa kwenye hili na hata kushirikishwa kwenye hii kampeni! BONTA .... HESHIMA YANGU NIPENI" Bonta Maarifa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad