Mshtakiwa namba moja wa mauaji ya rapper Nipsey Hussle yaliotokea March 31,2019 Mjini Los Angeles nje ya duka lake la ‘The Marathon Clothing’, Eric Holder’29 alipandishwa kortini siku ya jana April 4,2019 kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Inaelezwa kuwa kesi ya Eric Holder inasimamiwa na mwendesha mashtaka maarufu nchini Marekani Christopher Darden, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa miaka ya 90 baada ya kufanikiwa kuimaliza kesi kubwa ya mauaji iliyokuwa ikimkabili Mtangazaji Orenthal James Simpson.
Wakili huyo aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa huyo Eric Holder hana hatia na ametoa malalamiko kuhusu vyombo vya habari kuruhusiwa kuingia mahakamani wakati wa kesi hiyo ikiendelea.
Mshtakiwa wa kwanza wa mauaji ya Nipsey Hussle Afikishwa Mahakamani
0
April 05, 2019
Tags