Mwanafunzi mmoja anayesomea masuala ya TEHAMA nchini Afrika Kusini, Bright Chabota anasakwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za kudukua data za serikali katika Sekta ya Afya na kisha kujiajiri mwenyewe.
Duru za habari nchini humo zinaeleza kuwa, Bright amekuwa akipokea mshahara bila kufanya kazi kuanzia mwezi Juni mwaka jana.
Bright Chabota inaarifiwa kuwa hakuwahi kwenda kazini ila amekuwa akipokea mshahara kila mwisho wa mwezi.
Chabota amegundulika baada ya serikali kukosa rekodi za malipo ya kodi kutoka kwake, ikiwemo ada ya bima ya matibabu nchini humo.
Tayari wazazi wake wamehojiwa na wamesema kuwa mtoto wao aliwataarifu kuwa ameshapata ajira serikali na analipwa mshahara mnono.
Kwa mujibu wa mtandao wa Zambian Observer, kila Chabota alikuwa akijilipa Randi 7000 kwa mwezi ambayo sawa na Tsh Milioni 1.2 .
Msomi Adukua Mtandao wa Serikali na Kujiajiri Mwenyewe, Ajilipa Mshahara Mnono kwa Miezi 9
0
April 15, 2019
Tags