Mtanzania ateuliwa na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis kuwa balozi wake nchini New Zealand

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amemteua Askofu Novatus Rugambwa mzaliwa wa Parokia ya Ishwandimi, Bukoba vijijini, Jimbo katoliki la Bukoba kuwa balozi wa Papa nchini New Zealand.


Awali Askofu Novatus Rugambwa alikuwa balozi wa Papa Francis nchini Honduras.

Askofu Rugambwa ni moja ya Watanzania wakatoliki ambao wamewahi kupata cheo kikubwa cha uongozi katika kanisa katoliki, Baada ya Kardinali Laurean Rugambwa, Kardinali Pengo, na Askofu Protace Rugambwa mkuu wa uinjilishaji ulimwenguni na mshauri wa Papa huko Vatican.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad