Mtoto wa Waziri Mkuu Asimama Upande wa CAG

Mtoto wa Waziri Mkuu asimama upande wa CAG
Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika vya Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika,  Dk Mwele Malecela amesema Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Prof  Mussa Assad, ni kati ya watu ambao histori itawakumbuka kama mtu wa heshima  Tanzania.

Dk. Malecela ameweka wazi hayo zikiwa ni siku mbili kupita tangu Bunge la Tanzania kupitisha kutofanya kazi na CAG kutokana na kauli yake 'Bunge ni dhaifu' kwa madai ilikuwa na lengo la kulidhalilisha Bunge hilo.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Dk. Mwele ameandika kuwa yeye anasimama na CAG kwa kuwa ameweza kuonyesha bado kuna watu wakamilifu na yeye Assad akiwa ni mmoja wapo hasa katika kipindi hiki ambacho historia inaonyesha kwamba taifa lipo katika wingu jeusi.

Dkt Mwele ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu, John Samuel Malecela amemwambia Prof Assad kwamba, "Historia itakukumbuka kama mtu wa heshima".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad