Muungano wa G7 na Umoja wa Mataifa Walaani Mapigano Mapya Libya

Mataifa yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani G7, pamoja na Umoja wa mataifa yamelaani vikali mapigano yaliozuka upya nchini Libya.

Mataifa hayo yanataka pande zinazohasimiana Libya "kusitisha mara moja shughuli za kijeshi". Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa wito huo.

Tripoli ni makao makuu ya serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa, na ambayo pia inaungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.


Vikosi vya kulinda usalama vya umoja wa mataifa katika mji huo vimekuwa katika hali ya tahadhari.

Ghasia zimekumba Libya tangu utawala kiongozi wa nchi hiyo wa mda mrefu, Muammar Gaddafi kuangushwa na yeye kuuawa mwaka 2011.

Nini kinachofanyika?

Kamanda Khalifa Haftar, ambaye ni kiongozi wa vikosi vya kijeshi vinavyopinga utawala wa Tripoli siku ya Alhamisi aliamuru vikosi vyake kuingia mji wa Libya.

Hatua hiyo ilijiri wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akiwa mjini humo kujadili mzozo unaoendelea sasa.

Kumeripotiwa mapigano karibu na uwanja wa kimataifa wa ndege uliyopo kusini mwa mji huo.

Jenerali Haftar alikuzungumza na Bw. Guterres mjini Benghazi siku ya Ijumaa, na inaripotiwa kuwa alimwambia kiongozi huyo kuwa oparesheni yake haitakomeshwa hadi pale vikosi vyake vitakaposhinda "ugaidi".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad